Bongo Fc


Dani alves bado anatamani kucheza ligi ya uingereza

Beki wa Paris Saint-Germain Dani Alves amekiri kuwa bado anatamani kucheza Ligi Kuu Uingereza kabla ya kustaafu soka.

Beki huyo wa Kibrazili alikaribia kujiunga na Manchester City ya Pep Guardiola majira ya joto, kabla ya kuamua kujiunga na miamba wa Paris, uhamisho uliowashangaza City.

"Kulikuwa na mambo mengi ya kuangalia, na nililazimika kutua PSG," mkongwe huyo wa miaka 34 aliiambia FourFourTwo. "Guardiola ni sababu kubwa, kuliko zote, ambazo zingenishawishi kujiunga na Manchester City.

"Mwishowe, kulikuwa na fursa ya kuungana na marafiki zangu PSG, katika jiji lenye mvuto na klabu yenye sifa. Natambua kwamba naweza kuongeza ubora katika klabu zaidi ya soka.

"Ilinigusa zaidi kuichagua PSG badala ya City kwa sasa, Lakini sitaki kuficha hisia zangu kuwa namkubali Pep na nia yangu kucheza Ligi Kuu Uingereza siku za mbeleni."

Alves ni mshindi wa taji la Ligi ya Mabingwa mara tatu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.