Bongo Fc


Shearer: uchoyo utamsaidia lukaku kupata mafanikio old trafford

Mshambuliaji nyota wa Manchester United, Romelu Lukaku ametakiwa kuwa mchoyo ili kupata mafanikio Old Trafford.

Lukaku, ametakiwa kuwa mchoyo wa kutoa pasi ili kupata nafasi ya kufunga mabao, vinginevyo atakuwa katika mazingira magumu Man United.

Alisema Lukaku mwenye miaka 24, hawezi kufunga mabao kama atakuwa akikimbilia eneo la kibendera na kuacha nafasi ya ushambuliaji wa kati.

Kauli hiyo ilitolewa na nguli wa zamani wa England, Alan Shearer alipochambua mchezo baina ya Man United na Chelsea. Man United ilifungwa bao 1-0 ugenini Uwanja wa Stamfotrd Bridge, lililofungwa na mshambuliaji wa Kihispania Alvaro Morata.

Shearer alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji anapata wakati mgumu kufunga mabao kwa kuwa 'halishwi' mipira kikamilifu. Alisema Lukaku amekuwa akifanya kazi kubwa ya kutafuta mipira na kutoa pasi za mwisho kwa wenzake, hatua ambayo inamgharimu.

"Nadhani anatakiwa kuwa mchoyo kwasababu yeye kazi yake ni kufunga mabao si kupika mabao, amekuwa akiingia ndani ya eneo la hatari lakini ana kazi ya kutoa pasi za mwisho," alisema Shearer kwenye mahojiano na SkySports.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa Man United majira ya kiangazi kutoka Everton, ameshindwa kufunga bao katika mechi saba.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.