Bongo Fc


Mke wa rooney akubali yaishe

Mke wa straika wa Everton, Wayne Rooney, Coleen Rooney, ni kama amekubali yaishe, baada ya kumsamehe mumewe na kumruhusu waishi tena pamoja.

Coleen ambaye kwa sasa ni mjamzito, alitangaza kumtosa mumewe Septemba mosi baada ya staa huyo wa zamani wa Man Utd kukamatwa na polisi akiwa amelewa na huku akiendesha gari ya mwanamke mwingine.

Wakati wa tukio hilo, mwanasoka huyo anadaiwa alikuwa akimkumbatia na kumbusu kimwana huyo hadi wanakamatwa na polisi.

Hata hivyo, baada ya miezi takribani miwili ya mvutano sasa hali ya amani inaonekana kurejea ndani ya familia ambapo juzi Rooney alituma picha kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter zikimwonesha akiwa na familia yake wakati wakifanya maandalizi ya siku ya kuzaliwa mtoto wao wa kwanza, Kai.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.