Bongo Fc


Kumbe chelsea wangeifunga man united kivyovyote

Na: Omary Ramsey

Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka kati ya Manchester United waliokuwa Stamford Bridge kukabiliana na wenyeji wao Chelsea, ulimalizika kwa Mashetani Wekundu hao kuchapwa bao 1-0.

Chelsea waliofungiwa bao pekee na staa Alvaro Morata, waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 3-0 na Roma katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wachambuzi wa soka barani Ulaya wameibua sababu zilizowafanya Man United kushindwa kuambulia walau sare katika mchezo huo wa juzi licha ya kuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Rekodi za Man United wakiwa Stamford Bridge

Man United hawana rekodi nzuri ya kuondoka Stamford Bridge na kicheko. Timu hiyo ya jijini Manchester imepoteza mechi 17 kati ya 22 za Ligi Kuu dhidi ya Chelsea kwenye uwanja huo, huku ikiruhusu mabao 66.

Kwa kipindi cha miaka 17 iliyopita, yaani tangu mwaka 2000, Man United wameshinda mechi mbili pekee pale Stamford Bridge.

Majeraha Man United

Kikosi cha Man United kilichopata ushindi wa mabao 4-0 katika mechi sita za mwanzo wa msimu huu, si hiki cha sasa. Tayari majeraha yamekifanya kuwapoteza Paul Pogba, Marouane Fellaini na Michael Carrick.

Licha ya uwepo wa Ander Herrera na Nemanja Matic, bado mashabiki wa Man United wanakiri kuwa eneo la kiungo la timu yao haliko sawa kama alivyokuwapo Pogba.

Safu ya ushambuliaji Man United

Tangu Pogba alipoumia katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Basel, safu ya ushambuliaji ya Man United imeonekana kupoteza makali yake.

Kocha Jose Mourinho amekuwa akimtumia Henrikh Mkhitaryan kama mchezeshaji wa timu, lakini bila Pogba, nyota huyo ameshindwa kutekeleza vizuri jukumu lake hilo.

Kurejea kwa N’Golo Kante

Kupotea kwa Chelsea katika mechi za hivi karibuni kulitokana na kukosekana kwa kiungo Kante, lakini juzi alikuwa uwanjani na kuthibitisha umuhimu wake kikosini.

Kante amekuwa akitekeleza vema jukumu lake la kuwalinda mabeki watatu, hivyo kuifanya safu ya ulinzi ya kocha Antonio Conte kuwa imara zaidi.

Kukosekana kwake kuliifanya Chelsea kumtegemea Tiemoue Bakayoko katika eneo la kiungo wa ulinzi. Lakini sasa, Bakayoko amekuwa na kawaida ya kuvutwa na mashambulizi, huwa anasogea zaidi na kuliacha jukumu la kudumisha ulinzi.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.