Bongo Fc


Straika mbeya city: haturudii makosa

Mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile, amesema hawatarajii kurudia makosa katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga, mtanange utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ambokile mwenye mabao manne katika orodha ya wafungaji, amesema makosa waliyoyafanya dhidi ya Simba ‘Wekundu wa Msimbazi’ hayawezi kujirudia watakapokuwa ugenini kucheza dhidi ya mabingwa watetezi Yanga.

Akizungumza na BongoFC, Ambokile alisema katika mchezo uliopita walitengeneza nafasi nyingi ambazo walishindwa kuzitumia, hivyo anaamini kipindi hiki watatumia muda huo kurekebisha makosa.

“Ulikuwa mchezo mgumu kwetu licha ya kuwa tulikuwa nyumbani, kwani tulikuwa tunacheza na timu kongwe na yenye uzoefu mkubwa ingawa tulijitahidi kupambana,” alisema.

Ambokile ambaye ameitwa katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 23, alisema malengo yake msimu huu ni kufanya vizuri zaidi ikiwezekana kuendelea na kasi hiyo ya upachikaji mabao ili aweze kutwaa kiatu cha ufungaji bora.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.