Bongo Fc


Kichuya atoa neno kwa washambuliaji bongo

Winga wa Simba, Shiza Kichuya amesema ugumu wa Ligi Kuu Bara, unasaidia wachezaji kujituma na kuwataka washambuliaji wa Kitanzania kuchukua tuzo ya ufungaji bora msimu huu.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji muhimu Simba, waliofanikisha iwe kileleni kwa pointi 19 sawa na Azam wakitofauti wa mabao.

Kichuya mfungaji wa bao pekee dhidi ya Mbeya City mwishoni mwa wiki alisema ugumu wa ligi unamsaidia kujituma kwa bidii kuanzia mazoezini hadi uwanjani, kuhakikisha timu yake inakuwa na mafanikio ya juu.

"Siyo kwa sababu nimefunga, Simba tunacheza kwa umoja na kujituma, hakuna ambaye anataka acheze kwa maslahi yake mwenyewe, ndiyo maana nasema ugumu unaongeza maarifa kwa mchezaji, akijua wazi kwamba wapinzani wanakuja kwa kasi,"alisema.

Ugumu wa ligi hiyo, anashauri uwe somo kwa wachezaji wazawa hasa upande wa washambuliaji, kuhakikisha kiatu cha ufungaji bora, anachukua mzawa ili kurejesha heshima kama ilivyokuwa kwa kina Edbliy Lunyamila na Zamoyoni Mogella.

"Siyo lazima nichukue mimi, kinaweza kwenda kwa mzawa yoyote, kama ilivyokuwa kwa Simon Msuva ambaye kwa sasa yupo Morocco pamoja na Abdulrahman Mussa,"alisema Kichuya.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.