Bongo Fc


Hatimaye moyes awa amrithi bilic west ham

West Ham wamekua na mwanzo wa kusuasua katika Ligi Kuu msimu huu na sasa wamemgeukia kocha wa zamani wa Everton kuwanusuru kushuka daraja.

West Ham wamemchagua David Moyes kuwa meneja wao mpya baada ya kuachana na Slaven Bilic.
The Hammers wapo nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu baada ya kipigo cha 4-1 mikononi mwa Liverpool wikendi iliyopita.

Na baada ya kipigo hicho wakafikia maamuzi ya kuachana na Kocha huyo ambaye pia almanusura wamteme msimu uliopita pia ambapo aliambulia nafasi ya kumi na moja katika ligi.

Moyes alikua hana kibarua tangu ajiuzulu kuifundisha Sunderland ambayo nayo ilishuka darajani ikiwa mikononi mwake msimu uliopita.

Mskotishi huyu hajawa na matokea chanya katika timu alozfundisha tangu aachane na Manchester United aliyoifundisha kwa miezi tisa tu kabla hajatupiwa virage na nafasi yake kuzibwa na Mholanzi Van Gaal.

Waginga nyundo hao wa London watarudi tena dimbani tarehe 19 Novemba watapovaana na Watford.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.