Bongo Fc


Wenger ajipa moyo giroud kurudi uwanjani

Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud atakosa mchezo wa kimataifa baada ya kuumia kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa.

Giroud juzi jioni alishindwa kuendelea na mazoezi baada ya kupata maumivu ya mguu wakati Ufaransa ikijiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Wales utakaochezwa Ijumaa wiki hii.

Mchezaji huyo alionekana akigugumia kwa maumivu akiwa ameshika sehemu ya chini ya ugoko ingawa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps ana matumaini atarejea uwanjani mapema kwa kuwa hakupata majeraha makubwa.

Pia kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger, alisema Giroud hakupata majeraha ambayo yanaweza kumuweka benchi muda mrefu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.