Bongo Fc


Bila samatta, stars kuwafuata benini kesho

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kuondoka kesho Alhamisi kwenda nchini Benin kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya Fifa.

Taifa Stars inakwenda Benin bila ya nahodha wake, Mbwana Ally Samatta ambaye ameumia goti na atatakiwa kukaa nje kwa wiki sita akipata matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alisema kuwa wachezaji wote wameshaingia kambini kasoro nahodha, Mbwana Samatta ambaye ni majeruhi pamoja na Abdi Banda.

“Kikosi cha timu yetu ya taifa kinatarajia kuondoka hapa keshokutwa (kesho), Novemba 9, alfajiri kwenda Benin kwa ajili ya mechi yao ya kimataifa ya kirafiki na kitakapofika rasmi kesho yake kitaendelea na programu yake mazoezi huko Benin,” alisema Lucas.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.