Bongo Fc


Salah hakamatiki liverpool msimu huu

Na: Omary Ramsey

Liverpool imelamba dume kupata saini ya kiungo wa pembeni Mohamed Salah, katika usajili wa majira ya kiangazi.

Kauli hiyo imetolewa na mchambuzi wa soka na beki wa zamani wa timu hiyo Jamie Carragher, aliyekuwa akimzungumzia mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri.Carragher alisema Liverpool imefanya usajili wa maana na fedha zake zimetumika kikamilifu kutokana na kiwango bora cha mshambuliaji huyo.

Mchambuzi huyo alisema Salah anaweza kufunga mabao 25 msimu huu kwa kuwa ni mchezaji hodari mwenye kiwango bora cha soka.

Mechi 16 za michuano tofauti alizocheza Salah zimempa nafasi ya kuwemo katika kikosi cha kwanza Liverpool inayonolewa na Mjerumani Jurgen Klopp.

Salah alianza kuipa Liverpool karamu ya mabao katika mshindi wa 3-0 katika mchezo w Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Maribor uliopigwa katikati ya wiki.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.