Bongo Fc


Msuva: yanga itakua mabingwa msimu huu

Winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva pamoja na mambo mengine ameitabiria timu yake ya zamani ya Yanga kutwaa taji la Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu.

Msuva anayesakata kandanda kwenye klabu ya Jadida ya nchini Morocco amesema kwamba licha ya kucheza soka ughaibuni lakini huwa anaifuatilia Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa njia ya simu.

Winga huyo amesema kuwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara imekuwa ngumu sana msimu huu lakini anaamini timu yake ya Yanga itafanikiwa kuwa mabingwa msimu huu.

Msuva aliisaidia Yanga msimu uliopita kutwaa taji la Ligi Kuu Bara baada ya kufanikiwa kuwa mfungaji bora ndani ya kikosi hicho na Ligi Kuu kwa ujumla.

“Sio tu kuifuatilia, huwa naiangalia kupitia njia ya simu, kiukweli ligi imekuwa ngumu sana msimu huu, ni timu yangu kwanini sasa nitiitabirie mazuri, naamini Yanga itakua mabingwa msimu huu,” alisema Msuva kwenye mazoezi ya Taifa Stars.

Winga huyo yupo nchini Tanzania ambapo amekuja kujiunga na kambi ya timu ya taifa ya Tanzania itakayocheza dhidi ya Benin Novemba 12.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.