Bongo Fc


Lewandowski: bayern lazima ikubali kusajili wachezaji bora

Nahodha wa timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski amesema klabu yake ya Bayern Munich ni lazima isajili wachezaji waliyobora kila msimu ili kuweza kuleta ushindani wa kweli ndani na nje ya timu.

Lewandowski ambaye yupo na timu ya taifa kujiandaa na michezo ya kirafiki dhidi ya Uruguay siku ya Ijumaa na Mexico Jumatatu hijayo ameyasema hayo kupitia mahojiano na Reuters.

“Tusijidanganye kila klabu inahitaji kupata wachezaji waliyobora kila baada ya miaka miwili ama mitatu ili kuimarisha timu, kuleta damu mpya na viwango vingine kuifanya timu kuwa na uhai.” Amesema Lewandowski.

Mwanzoni mwa msimu mpya Bayern ilimtimua kocha wake raia wa Italia, Carlo Ancelotti na kumrejesha Jupp Heynckes mwenye umri wa miaka 72 kitendo ambacho kinaonekana kuzaa matunda.

Tangu kocha Heynckes arejee ndani ya kikosi hicho Oktoba 14, timu hiyo imeshinda jumla ya michezo saba katika mashindano yote huku ikirejea nafasi ya juu katika ligi ya Bundesliga ikiziacha RB Leipzig na Borussia Dortmund chini.

Jupp Heynckes akiiwezesha kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Lewandowski ameongeza “Kwa wakati huu tuna timu nzuri lakini nilazima tufahamu kuwa wachezaji umri wao unazidi kwenda. Tunafanikiwa leo kwa kuwa tuna wachezaji vijana, Josh Kimmich ambaye ni mzuri katika nafasi yake.”


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.