Bongo Fc


Waghana wazifilisi simba, azam

Utamaduni wa klabu za Simba na Azam kutafuta wachezaji wa nafasi za ushambuliaji kutoka nchini Ghana, limewatokea puani baada nyota waliosajiliwa kutoka nchini humo kuchemka vibaya.

Simba imeingia kwenye hasara kubwa baada ya straika Mghana, Nicholas Gyan ambaye ameigharimu klabu hiyo zaidi ya Sh60 milioni kutokana na fedha za usajili pamoja na mishahara yake klabuni hapo.

Azam, jana Jumanne ilitangaza kuachana na straika Mghana, Yahya Mohammed ambaye
ameigharimu Azam zaidi ya Sh 120 milioni kutokana na gharama za usajili pamoja na mishahara ya mwaka mmoja.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.