Bongo Fc


Vita ya usajili dirisha dogo kuzikumba simba, yanga

Dirisha dogo la usajili linafunguliwa wiki ijayo, huku viongozi wa timu wakianza kuwindana ili kudaka wachezaji nyota kwa ajili ya kuongeza makali kwenye vikosi vyao.

Simba inaongoza ikiwa na alama 19 sawa na Azam lakini wakiwa na faida ya uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, wakati Yanga yenyewe ina pointi 17 kama za Mtibwa Sugar, ila uwiano wa mabao unawabeba mbele yao.

Yanga iliyolazimishwa sare mbili mfululizo katika mechi zao zilizopita ikiwa ile na watani zao Simba walifungana nao bao 1-1 kabla ya Singida United kuibana na kutoka nao suluhu, imeachwa pointi mbili na Simba katika msimamo wa ligi.

Kocha Lwandamina ameuambia uongozi kuwa, katika dirisha dogo anataka mastraika mawili tu wa kuimaliza Simba.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.