Bongo Fc


Neymar hana furaha psg, real madrid yajipanga kumng’oa

Raisi wa Klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ameanza kuonesha nia ya kumuhitaji mchezaji wa Kibrazil, Neymar Jr ili kuziba pengo la nyota wake, Cristiano Ronaldo.

Neymar amejiunga na PSG msimu huu akitokea kwa wapinzani wakubwa wa Madrid, klabu ya Barcelona kwa uhamisho wa rekodi ya Dunia ya paundi milioni 200 ndizo zilizotumika kumg’oa Catalunya Mbrazili huyo.

Ripoti zinasema kuwa nyota huyo anajuta kujiunga na miamba hiyo ya Ufaransa, kwani kumekuwa na tetesi kuwa Neymar hana mahusiano mazuri na Edson Cavani pamoja na mwalimu wake Unai Emery tangu ajiunge na klabu hiyo.

Real Madrid ndio walikuwa wa kwanza kuulizia huduma ya Neymar kabla ajajiunga na Barcelona mwaka 2013, na sasa wanamtaka kwa mara nyingine kuja kurithi mikoba ya Cristiano Ronaldo.

Ronaldo ndie mfungaji bora wa Madrid baada ya kufanikiwa kufunga magoli 414 katika mechi 407 tangu ajiunge na Madrid 2009, lakini sasa ana umri wa miaka 32 na kasi yake ya kufamnia nyavu imepungua kwani ana goli moja tu msimu huu katika michezo saba.

Fomu mbovu ya mshindi huyo wa tuzo 4 za Ballon d’Or ndiyo sababu ya kuwafanya Los Blancos kuanza kutafuta mchezaji ambaye ana uwezo wa kuziba nafasi ya nyota huyo, na Neymar anaonekana kama mbadala sahihi.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.