Bongo Fc


Morata: nataka kuweka historia chelsea

Straika wa Chelsea Alvaro Morata amesema kuwa anataka kujenga historia ndogo katika klabu hiyo kwa kuwa Muhispania wa kwanza kushinda taji Uingereza, Italaia na Hispania.

Morata alitwaa taji la ligi ya nyumbani katika misimu yote mitatu iliyopita, alitwaa mara mbili mfululizo akiwa Juventus kabla ya kuisaidia Real Madrid kuvua taji Barcelona msimu uliopita.

Usajili huo wa rekodi wa Chelsea sasa anataka kutwaa taji Stamford Bridge pia, ingawa amekiri kuwa itakuwa changamoto kwani Blues wapo nyuma ya Man City kwa pointi tisa tayari.

"Sijuti kujiunga na klabu kama Chelsea na natumaini kubaki hapa kwa muda mrefu," aliiambia Marca. "Hupaswi kuwa na majuto katika maisha, hatua zote nilizochukua katika soka zimenisaidi na nimejifunza kutokana nazo, Nilishinda Italia, nilishinda Real Madrid na niimejiona wa muhimu. Sasa nina changamoto mbele yangu kuwa bingwa Hispania, Italia na Uingereza.

Aliongeza, "Mmoja au Wahispania wachache wamefanikiwa kufikia hili na ni lengo langu. Kutwaa taji Ligi ya Uingereza na kuwa Muhispania aliyeshinda mataji katika nchi tatu tofauti."

Morata amefunga magoli nane katika mechi 13 tangu ajiunge na Chelsea majira ya joto.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.