Bongo Fc


Paul pogba mbioni kurudi dimbani

Habari njema kwa mashabiki wa Manchester United ni kwamba Pogba anarejea kuongeza makali ya Mashetani Wekundu.

Kiungo wa Manchester United Paul Pogba, mbioni kurejea mzigoni upesi baada ya kuuguza majeraha ya muda mrefu kwa mujibu wa habari.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 hajaichezea timu ya Mashetani Wekundu tangu alipoumia misuli ya paja katikati ya mwezi Septemba, na amekosa mechi 12 katika michuano yote.

Bosi wa United Jose Mourinho amethibitisha mapema wiki hii kuwa Pogba, pamoja na nyota mwenzake Zlatan Ibrahimovic watarejea kabla ya mwisho wa mwaka.

Kwa mujibu wa Daily Star, Mourinho kisiri-siri anaamini kuwa nyota huyo wa zamani wa Juventus atarejea baadaye mwezi huu, lengo kuu likiwa mechi ya Novemba 18.

Pogba, ambaye kukosekana kwake kumeifanya United kuwa nyuma ya Manchester City katika mbio za ubingwa Ligi Kuu Uingereza, anatarajiwa kurejea mazoezini wiki ijayo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.