Bongo Fc


Noma sana!! mastraika simba kila bao mil.14

Klabu ya Simba imejikuta katika hasara kubwa baada ya mastraika wake wanne wanaolipwa jumla ya Sh19.3 milioni kwa mwezi kufunga mabao manne tu tangu kuanza msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Mastraika hao ni Laudit Mavugo aliyefunga mawili, John Bocco na Juma Liuzio waliofunga moja kila mmoja pamoja na Nicholas Gyan ambaye hajafunga bao lolote msimu huu.

Nyota hao wanne ndiyo mastraika tegemeo Msimbazi, lakini kasi yao ya kupachika mabao hairidhishi baada ya kufunga mabao hayo manne tu katika mechi tisa, ikiwa ni wastani wa bao moja kila baada ya dakika 202.

Katika kipindi cha miezi mitatu ambayo wamecheza mechi hizo tisa, nyota hao wameigharimu Simba mishahara ya Sh57.9 milioni.

Hili linamaanisha kuwa kila bao lililofungwa na mastraika hao, limeigharimu klabu hiyo Sh14.4 milioni.

Bocco ndiye aliyeitia Simba hasara kubwa zaidi kwani katika kipindi hicho cha miezi mitatu, amechukua mishahara inayofikia Sh20 milioni huku akifunga bao moja tu.

Mavugo ambaye anahusishwa kujiunga na Gor Mahia ya Kenya, amekuwa na nafuu kwani katika kipindi hicho amelipwa mishahara ya Sh13.5 milioni na kufunga mabao mawili. Gyan ndiye aliyekula mshahara wa bure kwa kulipwa Sh16.5 milioni huku akiwa hajafunga kabisa.

Liuzio amechukua kiasi cha Sh7.2 milioni na kufunga bao moja tu katika kipindi hicho. Straika huyo wa zamani wa Zesco United ya Zambia hajafunga bao lolote tangu Agosti 26.

KUMBE KAWAIDA YAO

Huu umekuwa ni mwendelezo wa Simba kupata hasara kutoka kwa mastraika wake, kwani msimu uliopita, Fredrick Blagnon, aliondoka na pesa ndefu klabuni hapo bila kufunga mabao ya maana.

Blagnon aliyekuwa akilipwa Sh6.5 milioni kwa mwezi, alikaa Simba miezi 10 na kukusanya zaidi ya Sh65 milioni huku akifunga mabao manne tu katika mashindano yote. Hii ilimaanisha kuwa katika kila bao moja alilofunga Blagnon, lilikuwa na thamani ya Sh16 milioni.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.