Bongo Fc


Morata atoboa siri chelsea

Mshambuliaji Alvaro Morata amesema Zinedine Zidane ndiye aliyemshauri akajiunge na Chelsea badala ya Manchester United.

Mshambuliaji huyo usajili wake ulivunja rekodi huko kwenye kikosi cha Chelsea wakati ilipomnasa kwa ada ya Pauni 60 milioni kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi.

Morata, 25, alikaribia kabisa kujiunga na Man United kabla ya dili hilo kukwama na kutua Chelsea, ambako amefunga mabao manane katika mechi 14 alizoichezea timu hiyo yenye maskani yake huko Stamford Bridge.

Zidane aliwahi kusema kwamba hakufurahishwa na kitendo cha Real Madrid kumuuza Morata, lakini straika huyo amedai kwamba Mfaransa huyo ndiye aliyemshauri kwenda kwenye timu ambayo itampa muda wa kutosha wa kucheza.

"Nitamshukuru sana Zidane kwa sababu amenipa nafasi ya kushinda taji jingine la Ligi ya Mabingwa Ulaya nikiwa mchezaji wa Real Madrid," alisema Morata.

"Aliniambia ‘Alvaro, najua unataka kucheza na kuwa na kiwango, hivyo nadhani itakuwa jambo zuri kama utaondoka’. Aliniambia kwamba anataka nibaki, lakini ana machaguo mengi kwenye safu ya ushambuliaji. Hivyo nikaona kitu kizuri kwangu ni kuondoka, hasa ukizingatia unaelekea mwaka wa Kombe la Dunia na nilitaka kuwapo kwenye fainali hizo. Hivyo sijutii kuja Chelsea na nitakuwa hapa kwa muda mrefu."


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.