Bongo Fc


Mayanga: tutashinda ili kumfariji samatta

Kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga, amesema ametamba kuwa kikosi chake kinaweza kushinda mchezo dhidi ya Benin, bila uwepo wa nahodha na mshambuliaji Mbwana Samatta, ambaye hatokuwepo kwenye mchezo huo kutokana na kuwa majerui.

Mayanga ameiambia BongoFC, anakwenda Benin, akiwa anajivunia ukali wa washambuliaji waliopo kwenye kikosi chake ambao wanampa uhakika wa kushinda mchezo huo muhimu katika kujiweka katika mazingira mazuri ya kupanda kwenye viwango vya FIFA.

"Lazima nikiri kuwa Samatta, ni mchezaji muhimu kwenye kikosi changu, na kukosekana kwake kuna vitu tutavikosa, lakini uhakika wa ushindi katika mchezo huo upo palepale kwani ninaimani na washambuliaji niliokuwa nao kwenye kikosi changu," amesema Mayanga.

Kocha huyo amesema wamepanga kucheza kwa nguvu ili kupata ushindi ambao utamfariji Samatta, na kumfariji kwa kile kilichomkuta cha kuumia ambapo taarifa za daktari zinadai kuwa atakuwa nje kwa kipindi cha wiki sita.

Kikosi cha Stars, kinaondoka leo kuelekea Benin, kwa ajili ya pambano hilo la kirafiki ambalo limepangwa kupigwa Jumamosi ya keshokutwa huku Tanzania ikiwa na kikosi chake kamili akiwemo Simon Msuva anayechezea klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.