Bongo Fc


Man united bado kunafukuta

Romelu Lukaku ameingia katika mzozo na wachezaji wenzake wa Manchester United baada ya kipigo cha timu yao kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Lukaku, ambaye sasa ana miaka 24, alionekana kama aliyechanganyikiwa na kukasirishwa na jinsi walivyocheza na kushindwa kufunga kwa mechi saba sasa tangu mwezi uliopita.

Man United ilimaliza mchezo kwa kipigo cha pili cha Ligi Kuu England msimu huu baada ya kumwacha Alvaro Morata kuruka akiwa peke yake kufunga bao pekee la mchezo huo Jumapili iliyopita.

Lukaku anasemekana kuwa alikuwa akizungumza zaidi ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

Nyota huyo alikuwa akicheza mchezo wa kwanza katika uwana huo tangu alipojiunga na Man United kwa Pauni 75 milioni, baada ya kuonekana kama angejiunga tena na Chelsea akitokea Everton.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.