Bongo Fc


Omog adai atahakikisha analitumia dirisha dogo la usajili kukiboresha kikosi chake

Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog amesema atalitumia dirisha dogo la usajili kwa ajili ya kuziba nafasi chache zilizoonesha mapungufu kwenye mechi 9.

Mcameruni huyo amesema kikosi chake kitaongeza wachezaji wawili pekee katika dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa Jumatano ya wiki ijayo.

Omog ameiambia BongoFC, hiyo ni kutokana na uimara uliopo kwenye kikosi chake na mapungufu madogo yaliyojitokeza katika mechi tisa walizocheza kwenye mzunguko huu wa kwanza.

"Tuna mapungufu machache sana ndiyo maana nimesema tutaongeza wachezaji wawili ili kukiimarisha kikosi na kubalansi sehemu ambazo kidogo zilikuwa hizipo sawa," amesema Omog.

Kocha huyo raia wa Cameroon amezitaja nafasi za wachezaji ambao wanataka kuwakaribisha kuwa ni mlinzi wa kulia mmoja na mshambuliaji mwenye uwezo wa kucheza sehemu ya kiungo mmoja.

Amesema lengo lao ni kupata mtu ambaye atakuwa akisaidiana na washambuliaji waliopo huku pia kucheza kiungo mshambuliaji ili kuongeza ukali wa mashambulizi.

Simba pamoja na kuongoza ligi lakini kiwango chake bado kimeshindwa kuwafurahisha mashabiki wao na kulifanya benchi la ufundi kuumiza kichwa kwa kutafuta njia mbadala.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.