Bongo Fc


Ulimwengu kutua yanga

Wakati dirisha dogo la usajili Ligi Kuu Bara likitarajiwa kufunguliwa keshokutwa, Yanga iko mbioni kumsajili mshambuliaji wa zamani wa TP Mazembe ya Congo, Mtanzania Thomas Ulimwengu.

Ulimwengu anayekipiga kwenye klabu ya Athletic Football Club Eskilstuna ya Sweden, anatua Yanga kwa mkataba wa miezi sita ili kurejesha kiwango chake baada ya kutoka kwenye majeraha ya goti.

Mshambuliaji huyo kwa sasa yupo katika mazoezi maalamu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kurejea uwanjani kuitumikia Yanga katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa mwakani.

Na iwapo dili hilo litakamilika, ni wazi kuwa washambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib pamoja na Obrey Chirwa, watakuwa ni kama ‘wanamsukuma mvevi’ kwani hawatakuwa na kazi kubwa ya kupambana na mabeki wa timu pinzani wakimwachia Ulimwengu ambaye shughuli yake si ya kitoto.

Pamoja na uwezo wa hali ya juu alionao Ulimwengu katika soka, lakini pia anabebwa na nguvu zinazomwezesha kupambana na mabeki watemi kama Method Mwanjali wa Simba na wengineo, hivyo kuwafanya akina Ajib kubakiwa na kazi moja tu ya kucheka na nyavu.

Chanzo cha ndani kutoka Kamati ya Usajili Yanga, kimeidokeza BongoFC kuwa, Ulimwengu amepewa miezi sita ya kutafuta timu ya kurejesha makali yake na baadaye aweze kurejea klabuni kwake.

Taarifa kamili inakuja hivi punde..


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.