Bongo Fc


Hatimaye limetimia, afcon kupigwa miji minne bongo

Kazi imeanza. Miji ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Dar es Salaam ndiyo inapigiwa hesabu ya viwanja vyake kutumika kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali hizo za mwaka 2019 na tayari Serikali imekubali uenyeji huo na juzi Jumamosi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe alizindua Kamati ya Kitaifa ya mashindano hayo.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusufu Singo, amesema: “Tunategemea kuwapokea wataalamu kutoka CAF (shirikisho la soka la Afrika) wakati wowote kuanzia sasa, kikubwa wanachokuja kukifanya ni kukagua viwanja vitakavyotumika.

“Tunategemea kuwapeleka miji ya Mwanza, Arusha, Dodoma na Dar es Salaam kisha wao sasa ndiyo watashauri ni viwanja vipi ambavyo wanaona vinastahili kutumika kwenye AFCON na vitu gani vya kuboreshwa zaidi,” alisema Singo.

Akizungumzia maandalizi mengine, Singo alisema baada ya kamati kuundwa na kukutana katika kikao cha kwanza, wamekubaliana kukutana tena Jumamosi ijayo kwa ajili ya kupeana majukumu ikiwamo kupanga bajeti na kuanza harakati za kupokea ugeni.

Kama Tanzania itafanikiwa katika uenyeji huo, hayo ndiyo yatakuwa mashindano ya kwanza ya AFCON kuandaliwa hapa nchini tangu Uhuru mwaka 1961.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.