Bongo Fc


Wenger adaiwa yupo bize kusaka majembe

Kocha, Arsene Wenger ameripotiwa kwa sasa yupo bize kweli kutazama staa gani wa kumwingiza kwenye kikosi chake wakati wa usajili wa Januari.

Baada ya kushindwa kufanya usajili wa maana dirisha lililopita, huku akitambua mastaa wake kama Mesut Ozil na Alexis Sanchez wanaweza kuondoka itakapofika Januari, Wenger sasa anapambana kuhakikisha Arsenal inajibu mapigo kwa kushusha majembe ya maana kwenye kikosi hicho.

Wenger alimkosa staa wa Monaco, Thomas Lemar dirisha lililopita, lakini sasa atamrudia tena Januari ili kutengeneza kikosi kitakachokuwa tishio kwa wapinzani wao Ligi Kuu England na ligi nyingine.

Staa mwingine ambaye yupo kwenye rada za Wenger ni staa wa Lyon, Nabil Fekir, ambaye baba yake aliwahi kusema kama mwanaye ataondoka Ufaransa, basi atakwenda Arsenal.

Kwenye orodha hiyo ya Wenger yupo pia Mjerumani, Leon Goretzka, ambaye ni kiungo wa Schalke huku akimtaka pia fowadi wa PSG, Julian Draxler pamoja na kipa wa Real Madrid, Keylor Navas.

Maisha ya Draxler yamekuwa magumu huko PSG kutokana na kikosi hicho kufanya usajili wa mastaa wa maana, akiwamo Kylian Mbappe na Mbrazili Neymar wanaomfanya kukosa nafasi ya kutosha ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Wenger anamtaka kipa Navas pia kuja kuchukua mikoba ya makipa waliopo kwenye kikosi chake kwa sasa, Petr Cech na David Ospina baada ya kuona wamekuwa wakifungwa mabao mepesi sana.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.