Bongo Fc


Marseille yamtupia virago evra

Beki Patrice Evra ametimuliwa na klabu yake ya Marseille huku Uefa ikimfungia miezi saba kwa kumpiga teke la kung-fu shabiki.

Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) limeamua kuchukua hatua kali kwa beki huyo wa zamani wa Manchester United baada ya kubainika kufanya kitendo cha kumpiga teke shabiki kabla ya kuanza kwa mechi mwanzoni mwa mwezi huu.

Adhabu hiyo inamaanisha Evra hatoweza kucheza mechi za mashindano yoyote ya Uefa hadi Juni 30 2018, na sasa hatokuwa na klabu yoyote baada ya Marseille kuamua kuachana naye kufuatia adhabu hiyo.

Tukio hilo la kushangaza lilitokea kabla ya kuanza kwa mchezo wa Europa Ligi kati ya Marseille dhidi ya Vitoria uliofanyika Novemba 3.

Evra alipandwa na hasira wakati wa kufanya mazoezi na kikundi cha mashabiki wa Marseille waliokuwa pembeni yao walipokuwa akimrushia maneno ya kejeli.

Baada ya tukio hilo kulisababisha mashabiki hao na baadhi ya wachezaji kuanza kugombana pembeni ya uwanjani kabla ya Evra kumpiga teke shabiki huyo.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.