Bongo Fc


Kwa nini mourinho atasepa man utd

Na: Omary Ramsey

Tayari kumeanza kuzuka tetesi kuwa Jose Mourinho hatamaliza mkataba wake ?Manchester United, na kwamba anajiandaa kuachia ngazi.

Licha ya kwamba ndiyo kwanza ana mechi 11 tu za ligi katika msimu huu mpya, taarifa mara kwa mara zimezidi kudai kuwa Mourinho amekatishwa tamaa kutokana na baadhi ya matukio na anaweza kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu.

United ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England, lakini kwa sasa ipo pointi nane nyuma ya mahasimu zao Manchester City waliopo kileleni na katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wanaongoza kundi lao baada ya kushinda mechi zote nne.

Taarifa hizo pia zimedai kuwa kocha huyo raia wa Ureno hajaridhika kuhusu kusaini mkataba mpya Old Trafford.

Madai kwenye vyombo vya habari ni kwamba kuna sababu nyingi zinamfanya Mourinho kuwa na uwezekano wa kuondoka Old Trafford, na zimeainishwa na mwandishi, Tom McDermott.

Aliandika katika mtandao wa Twitter: "Jose Mourinho ameripotiwa kukatishwa tamaa na baadhi ya mambo yanayoendelea MUFC na anaweza kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Je, ni baada ya kuongeza mkataba? Hakuna uhakika. Fikiri muda aliotumia kumpata Matic katika mstari, kushindwa kusaini wachezaji wanne ni sababu.PSG, Hoteli

Licha ya kusajiliwa kwa rekodi ya dunia, kiasi cha pauni milioni 200, majira haya ya joto, baba mzazi wa Neymar, amefanya mazungumzo na Real Madrid kuhusu uwezekano wa mwanawe huyo kujiunga na Real Madrid kwa siku zijazo, kwa mujibu wa Gazeti la Mundo Deportivo la Hispania.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona, alihusishwa sana na kujiunga na Real Madrid kabla ya kuamua kufanya Catalunya kuwa nyumbani kwake wakati akihama kutoka Santos ya Brazil mwaka 2013.

Neymar ni wazi anataka kupata mafanikio binafsi, baada ya kukimbia kivuli cha Lionel Messi, na ni wazi atahitaji kurejea tena Hispania kutokana na ligi ya Ufaransa kutokuwa na ushindani mkubwa ukilinganisha na ligi zingine nne kubwa Ulaya.

Lakini pia Neymar anadaiwa kutofurahishwa na mbinu za kocha Unai Emery, hivyo Paris St-Germain, ipo tayari kumteua kocha Mourinho, kuinoa klabu hiyo ili kuongeza nafasi ya kumbakisha Mbrazili huyo.

"Pia chukulia kupigwa picha hadharani na PSG katika wiki za hivi karibuni na mashabiki kumsumbua. Kuendelea kukaa hotelini (The Lowry), ama London na familia yake.

"Pengine na sababu nyingine pia, lakini sitashangaa kuona akiondoka mwishoni mwa msimu," anaeleza McDermott.Historia

Mourinho mara zote amekuwa akipata mafanikio katika klabu msimu wake wa pili - alitwaa ubingwa wa ligi akiwa Porto, Chelsea, Inter na Real Madrid, lakini atashuhudia kazi yake ikikatishwa wakati huu Manchester City ikionekana kuwa imara.

Ed Woodward tatizo

Licha ya Mashetani Wekundu hao kuvutia chini ya Mourinho, taarifa zinadai kuwa kuna mambo nyuma yake hayamfurahishi Old Trafford, na moja likiwa ni kutokuwa na furaha na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward.

Inadaiwa kuwa Mourinho amepoteza imani na Woodward, hususan katika uwezeshwaji jambo ambalo linaweza kumfanya kukataa mkataba mpya.

Mourinho ambaye alitua Manchester United Mei mwaka jana, bado hajafanya mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba wake wa miaka mitatu aliosaini awali Old Trafford wakati huu kocha huyo wa zamani wa Real Madrid na Chelsea akihusishwa na kutua Paris.

Aliliambia Gazeti la Telefoot: "Kitu pekee ninachoweza kusema ni kwamba bado ninafundisha kwa hofu, malengo, hamu ya kufanya mambo mapya. Ninauhakika sitamalizia wasifu wangu hapa (na Manchester United).

"Watoto wangu ambao wanaishi London wanakwenda Paris kuangalia mechi ya Paris Saint-Germain na hawaendi Manchester. "Kwa nini Paris? Kwa sababu kuna kitu fulani cha kipekee. "Asili, ubora, vijana, ni wa kushangaza.’


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.