Bongo Fc


Lukaku adai kurejea kwa zlatan kutaongeza matumaini ya kushinda ligi

Na: Omary ramsey

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku amesisitiza kuwa kureje kwa Zlatan Ibrahimovic atakuja kufufua matumaini ya kushindwa ubingwa wa Ligi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 hajacheza mechi hata moja kwa Mshetani hao wekundu tangu kusaini mkataba mpya wakati wa majira ya joto,na ameendelea kufanya mazoezi binafsi kwa ajili ya kujiimarisha baada ya kuumia jeraha kubwa mwezi Aprili.

Ibrahimovic, ambaye aliongoza chati ya ufungaji bora kwa United msimu uliopita na ndiyo ulikuwa msimu wake wa kwanza huko Old Trafford, anatarajiwa kurudi uwanjani kabla ya mwishoni mwa mwaka.

Alipoulizwa juu ya mchango anaoutarajia kutoka kwa nyota mwenzake , Lukaku aliiambia Sky Sports News: "Kurudi kwa Ibrahimovic atatusaidia kumfukuzia Manchester City. Aliongeza, "Unapokutana na timu kama sisi ni vigumu kwa wapinzani. Inanihamasisha kweli, kwa sababu yeye ni mchezaji mwingine mzuri kuongezeka kikosi."

United wanakamata nafasi ya pili nyuma ya Manchester City kwa tofauti ya alama 8 baada ya michezo 11 ya Ligi Kuu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.