Bongo Fc


Man u, psg vitani kumwania mauricio pochettino

Na: Omary Ramsey

Mourinho alishafunguka kuwa hana mpango wa kubaki Old Trafford muda mrefu, Unai Emery naye kiti kimekuwa cha moto PSG, klabu zote zinamtaka Pochettino.

Meneja wa Tottenham Hotspur Mauricio Pochettino ameibua vita baina ya Manchester United na Paris Saint-Germain.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 sasa amefanya maajabu tangu alipotua London Kaskazini miaka mitatu na nusu iliyopita, akiiongoza klabu hiyo kumaliza nafasi ya tatu na ya pili Ligi Kuu Uingereza misimu miwili iliyopita.Pochettino anaweza kuondoka klabuni hapo mwisho wa kampeni za msimu huu, hata hivyo, kwa mujibu wa Gazeti la Daily Express, limedai kuwa United na PSG zinataka kumtoa kocha huyo White Hart Lane.

Watumiaji wakubwa wa fedha PSG inasadikika kuwa wanatafuta bosi mpya kurithi mikoba ya Unai Emery, ambaye kibarua chake kipo matatani ikiwa atashindwa kuwaongoza miamba hao wa Ufaransa kutinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa.

United wana hofu ya kumpoteza Jose Mourinho, lakini pia miamba hao wa Paris wanaweza kupata fursa ya kumnasa kocha huyo wa Kireno kwani ni pia ni shabaha yao nambari moja ikiwa atapatikana.

Pochettino pia amehusishwa na kibarua cha Real Madrid wiki za hivi karibuni baada ya kuisaidia Spurs kushinda 3-1 dhidi ya mabingwa hao wa Ulaya mapema mwezi huu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.