Bongo Fc


Ngoma kutua yanga wakati wowote

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma anatarajia kurudi nchini kuitumikiaklabu yake wakati wowote kuanzia sasa, klabu hio imethibitisha.

Ngoma alikua nchini Zimbabwe akishughulikia masuala yake ya kifamilia na hivi sasa masuala hayo yanatajwa kumalizika.

Mshambuliaji huyo ameiambia klabu yake kuwa wakati wowote kuanzia sasa anaweza kurudi nchini kwani masuala yake ya kifamilia yamekwisha.

Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amethibitisha hayo na kuongeza kuwa ni mapema mno kumchukulia hatua za kinidhamu mshambuliaji huyo.

“Ngoma atarejea nchini wakati wowote kuanzia sasa, alikua akishughulikia masuala ya kifamilia na ametumia kuwa tayari yameshakwisha,” alieleza Dismas Ten.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.