Bongo Fc


Hatimaye liverpool yamng'oa nyota wa shalke 04, leon goretzka

Liverpool imeripotiwa kuwa imeshinda mbiyo ya kuinasa saini ya nyota wa Shalke 04, Leon Goretzka kwenye dirisha la mwezi Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye kiwango chake kinazidi kukua siku hadi siku huko nchini Ujerumani amekuwa akihusishwa na kujiunga na Ligi Kuu ya Uingereza huko nyuma.

Klabu za Chelsea, Tottenham Hotspurs na Arsenal nao wameonesha nia ya kumnasa Goretzka, lakini gazeti la habari la Hispania Don Balon limeripoti kuwa Liverpool imeshinda mbio hizo za kumnyakuwa nyota huyo.

Nyota huyo wa Ujerumani inasemekana atajiunga na Majogoo hao mwezi Januari katika dirisha dogo la usajili, pia Goretzka amefuta uwezekano wa kuhamia Barcelona kutokana na kutokufuraishwa na mkataba wa miamba hiyo ya Catalunya.

Ujio wa Goretzka unaweza kufungua mlango kwa Philippe Coutinho kuondoka Anfield na kwenda Barcelona au Paris Saint-Germain.

Goretzka tayari amefunga mabao manne katika mechi tisa za msimu huu katika Ligi Kuu Bundesliga hadi sasa.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.