Bongo Fc


Bakayoko: kante si bora kuliko mimi





Kiungo wa Chelsea Tiemoue Bakayoko amesisitiza kuwa mchezaji mwenzake N'Golo Kante 'si bora zaidi yake'.

Bakayoko, 23, aling'ara katika mechi ya Chelsea waliyoshinda 1-0 dhidi ya Manchester United kabla ya mapumziko ya kimataifa, lakini hakuitwa kwenye kikosi cha hivi karibuni cha Didier Deschamps.

Inasadikika kuwa mchezaji huyo wa zamani wa AS Monaco anapata wakati mgumu kuingia kwenye kikosi cha Ufaransa Kombe la Dunia 2018, lakini Bakayoko amedai kuwa yeye 'ni bora' sawa na wachezaji wanaowekwa mbele yake kwa sasa, ikiwa ni pamoja na Kante.

"Nimehuzunika. Naamini Kombe la Dunia ni lengo langu kuu. Nacheza kwenye klabu kubwa, Naamini nitapata upendeleo," Bakayoko aliwaambia waandishi. "Nadhani [Adrien] Rabito, Kante, [Blaise] Matuidi, [Coretin] Tolisso hawajanizidi chochote.

Aliongeza,"Nayaheshimu machaguzi ya kocha na pia nawaheshimu wachezaji walichaguliwa, wana kipaji na ni marafiki. Najivunia kwamba wamechaguliwa, ningependa kuwa nao. Lakini haimaanishi kwamba mimi ni mbovu zaidi yao."

Bakayoko amefunga mara mbili na kutoa pasi mbili za ogli katika mechi 15 alizocheza Chelsea msimu huu.


Facebook Twitter

Match Highlights                  

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.