Bongo Fc


Salah afukuzia mabao ya suarez

Fowadi mpya wa Liverpool, Mohamed Salah amejiweka kwenye wakati mzuri wa kuvunja rekodi ya mabao 31 iliyowekwa na Luis Suarez wakati alipoifungia klabu hiyo ya Merseyside katika msimu wake wa mwisho kabla ya kuhamia Barcelona.

Baada ya kutua Liverpool kwa ada ya Pauni 34 milioni katika dirisha lililopita, Salah ameonyesha kuwa mchezaji muhimu katika kikosi hicho cha Jurgen Klopp baada ya kufunga mabao 12 katika mechi zake 17 za kwanza za michuano yote klabuni hapo.

Kwa kasi hiyo, Salah sasa anatazamwa kuwa mchezaji mwafaka wa kwenda kuivunja rekodi iliyowekwa na Suarez huko Anfield.

Kabla ya hapo, mchezaji ambaye alikuwa na nafasi ya kwenda kuivunja rekodi hiyo alikuwa Philippe Coutinho, ambaye aliishia kufunga mabao 14 tu msimu uliopita.

Mashabiki wengi wa Liverpool walibeza usajili wa Salah kwenye dirisha lililopita hasa baada ya kumwona namna alivyofeli alipokuwa Chelsea, lakini sasa staa huyo wa Misri amebadili kila kitu na kuwaziba midomo mashabiki hao.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.