Bongo Fc


Basel kiboko ya mourinho





Na: Omary Ramsey

Kocha Jose Mourinho alikuwa na kikosi chake jijini Basel kwa mara ya kwanza baada ya miaka minne katika Ligi ya Mabingwa. Amefungwa tena.

Manchester United imefika Basel kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka sita. Wamefungwa tena.

Historia hiyo imejirudia jana usiku wakati Basel ilipopata bao la ushindi dakika 89 kwa kuifunga Man United ya Mourinho kwa bao 1-0, na kuharibu rekodi ya timu hiyo katika Kundi A, na kuiweka nafasi yao ya kufuzu kwa raundi 16 ikisubili mechi ya mwisho kuamua hatma yao.

Soma la hivi karibuni la Ligi ya Mabingwa ni kwamba Basel ni timu ngumu dhidi ya timu za England hasa wanapocheza kwenye Uwanja wa St. Jakob Park.

Man United imeukumiwa kwa makosa yao ya kushindwa kumaliza nafasi nyingi walizozipata katika mchezo huo ambao walikuwa wametalawa tangu mwanzo.

"Katika kipindi cha kwanza tulitakiwa kushinda mabao 5 au 6-0," alisema Mourinho. "Mechi ilikuwa rahisi kushinda."

Upepo ulibadilika katika kipindi cha pili, na kuonyesha kwamba ni timu moja inastahili kushinda kabla ya Michael Lang kufunga bao pekee. Nyota huyo wa Uswisi alifunga bao pekee akimalizia krosi ya beki wa kulia Raoul Petretta.

Bao hilo linafanana na lile alilofungwa Mourinho alipotembelea mji huo Novemba 2013 wakati Chelsea ilipochapwa bao 1-0 katika dakika 87.

"Katika mechi hii sikufikiri kuwa tutakuwa tumepiga shuti moja la kulenga lango. Tumecheza vibaya mechi hii," Mourinho alisema katika kipigo cha awali. "Leo ni tofauti kabisa. Leo kipindi cha kwanza tulikuwa vizuri katika kila idara."

Jambo zuri kwa Man United bado wanamechi moja ya kuwahakikishia kufuzu kwa hatua ya mtoano. Hakukuwa na nafasi ya pili kwa Man United chini ya kocha Alex Ferguson wakati walipofungwa 2-1 na Basel, na kutolewa Desemba 2011.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.