Bongo Fc


sababu 5 mourinho kumtaka beki umtiti

Na: Omary Ramsey

Baada ya kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 24 wa kutua Nou Camp majira ya joto yaliyopita, Samuel Umtiti, amethibitisha kwamba anaweza kushindana katika kiwango cha juu.

Barcelona kwa sasa ipo kileleni mwa La Liga ikiwa na pointi nne zaidi ya timu inayoifuatia, na kumi zaidi ya mahasimu wao Real Madrid wenye pointi 24 baada ya timu zote kushuka dimbani mara 12.

Umtiti, 23, amekuwa mchezaji muhimu kwa kikosi hicho cha kocha Ernesto Velverde, akikisaidia kuwa imara katika safu ya ulinzi – wakati huu Barca ikiwa imeruhusu mabao manne tu kwenye mechi 12 za mwanzo mwa msimu huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja wa ligi hiyo.

Kuna uwezekano Mfaransa huyo akapata nafasi kwenye kikosi cha Ufaransa kitakachoshiriki Kombe la Dunia kama ataendelea kuwa katika kiwango hicho, na uwezo wake anaoonyesha msimu huu ni sababu ya kutosha kwa Jose Mourinho kufanya liwezekalo majira ya joto kumpata. Hakika Umtiti atamgharimu sana, lakini ushirikiano atakaoutengeneza na Eric Bailly utakuwa wa mafanikio na wa muda mrefu.Hapa ni sababu tano kwa nini Mourinho atapaswa kumwaga mkwanja wa kutosha ili kuipata huduma ya Umtiti Old Trafford...

1. 'Upacha' na Bailly

Uliza shabiki yeyote wa Manchester United yupi beki bora katika kikosi chao na atasema Eric Bailly. Waulize ni nani wangependa kuwa 'pacha' wa Bailly, jibu linaweza kuwa tofauti. Lakini ukweli ni kwamba United inakuwa imara sana katikati ikianza na kumaliza na Eric Bailly, tofauti na hapo nafasi hiyo ikichezwa na wengine matokeo yake ni makosa kufanyika.

Wachezaji wote hao wawili wana miaka 23, ikiwa na maana watakuwa na muda wa kujiendeleza pamoja na ushirikiano mzuri utasonga mbele pamoja.

Mourinho pia katikati atahitaji mzoefu zaidi katika kikosi chake, lakini angalau hatawataka kucheza kama Phil Jagielka.

2. Mbadala Imara Kuliko Lindelof

Kufuatia kutua Old Trafford akitokea Benfica majira ya joto kwa pauni milioni 30, ukweli Victor Lindelof amepata wakati mgumu kuzoea Ligi Kuu England na kuchomoza katika kikosi cha kwanza cha Mourinho.

Msweden huyo bado hajapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwenye mechi ya Ligi Kuu England na amecheza mara mbili tu akitokea benchi, na mashabiki wengi wanadai kuwa Jose ana mpango wa kutumia staili mpya kwa kumchezesha Mkhitaryan.

Wakati Lindelof anapochezeshwa United, kumekuwa kujitokeza makosa, na kuwaacha mashabiki wakishangaa kwa nini walitoa pauni milioni 30 kumnunua.

Umtiti atawagharimu zaidi, lakini tayari ameshaonyesha ubora kote Lyon na Barca, ikiwa na maana ni ngangari zaidi.

3. Umri Wao

Kwa kutazama kiwango cha Umtiti, inaonekana hana kizuizi. Ana uwezo wa kutuliza presha na kucheza mpira kutoka nyuma, na kuwezesha kumiliki wakati wengine wakiwa waokoaji tu, ni mmoja mwenye ubora.

Kwa ujumla anaweza kuelezewa kama mchezaji wa mfumo wa Pep Guardiola, ingawa Mourinho atakuwa akitumai kwamba hatatua kwa wapinzani wao.

Kwa umri wake wa miaka 23, Umtiti anakaribia kupata mafanikio makubwa. Chini ya uongozi sahihi Mreno huyo, atakuwa mmoja wa wachezaji bora duniani ndani ya miaka michache.

4. Ubora wa Kiwango cha Juu

Akiwa Lyon na Barca, Umtiti ametwaa Coupe de France alipokuwa Ligue 1 na Kombe la Mfalme (Copa del Rey) akiwa La Liga.

Mfaransa huyu anajua nini anachotakiwa kufanya kutwaa mataji, na atakuwa akitumai kutwaa ubingwa wa kwanza wa ligi msimu huu, wakati huu Barca ikionekana kama inaweza kulibeba taji hilo kutoka kwa mahasimu wao.

United imeukosa ubingwa wa England kwa miaka minne sasa, kuondoka kwa Sir Alex Ferguson kumeiathiri miamba hiyo ya Old Trafford kuliko ilivyotarajiwa.

Umtiti utakuwa usajili bora kwa sasa na baadaye, na atakuwa ni mwenye njaa ya ubingwa wa Ligi Kuu England.

5. Biashara Nzuri Kuliko Varane

Umtiti na Raphael Varane wanaonekana kuwa ukuta imara katika safu ya ulinzi ya Ufaransa kwa baadaye, na wote wakistahili hilo. Wachezaji wote wamekuwa muhimu kwa klabu zao na hakuna hofu ya kushinda mataji mengi katika wasifu wao kisoka.

United imekuwa ikihusishwa na kuitaka huduma ya Varane kwa miaka mingi sasa, na wanaweza kuendelea kumhitaji yeye badala ya Umtiti. Hata hivyo, dili la kumpata Varane litakuwa zaidi ya uwezekano wa kumuona kipa David De Gea kuhamia Real Madrid.

Kipa huyo Mhispania amekuwa mchezaji bora wa United kwa miaka michache iliyopita, hivyo kumpoteza litakuwa pigo kubwa.

Umtiti anachukuliwa kuwa bora kama ilivyo tu kwa Varane, na dili hilo kwa mchezaji huyo wa miaka 23, litaipa United nafasi kubwa ya kumbakisha De Gea.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.