Bongo Fc


Mzambia mbioni kutua simba

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba wapo mbioni kumalizana na mshambuliaji wa Zesco United, Zambia, Jonas Sakuwaha.

Sakuhawa amewasili kwa majaribio katika kikosi cha Simba ambacho kitaanza mazoezi Ijumaa na atakuwa chini ya uangalizi wa kocha msaidizi Mrundi Masoud Djuma ambaye akisema freshi tu, jamaa anakula mkataba.

“Tumewaambia viongozi wasisajili mchezaji yoyote wa kigeni bila kumuona katika mazoezi na kama tutakuwa hatujaridhishwa na kiwango chake tutamuacha na tutahitaji mwingine na kama atapatikana aliyokuwa vizuri ndio tutawambia viongozi wamalizane nae,” alisema.

“Omog ataondoka na jukumu litabaki kwangu na tutakuwa tunawasiliana kwa kipindi chote ambacho hatakuwepo hapa ili kama atakuja asiwe na kazi kubwa ya kuanza kumuangalia upya wachezaji ambao watakuwa katika majaribio,” alisema Djuma.

“Sijamuona Sakuwaha lakini nimesikia kuwa tayari ameshaingia nchini lakini nitakuwa na taarifa zake rasmi baada ya siku ya Ijumaa nikishamuona katika mazoezi yetu,” alisema Meneja wa Simba, Richard Robert.

Sakuwaha alizaliwa Julai 22, 1983 katika Mji Kafue nchini Zambia anacheza nafasi ya mshambuliaji wa kati au pembeni na ni mzuri katika kufunga kokote ambapo kocha atampa nafasi ya kucheza.

Sakuhawa ni mchezaji mzoefu kwani amecheza kwa miaka tofauti Zesco United, Lorient ya Ufaransa, El Merreikh ya Sudan na TP Mazembe ya DR Congo.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.