Bongo Fc


Matola amruhusu kwasi atue simba

Kocha wa Lipuli FC, Suleiman Matola "Veron", amewaambia Simba kama wanamtaka beki wake wa kati Mghana, Asante Kwasi, kwenda kukamilisha mazungumzo haraka kwa sababu anajua atawasaidia kwenye mashindano ya kimataifa mwakani.

Kwasi ambaye ametua Lipuli akitokea Mbao FC ya Mwanza, alionyesha uwezo mzuri na kufanikiwa kuisawazishia timu yake bao katika mechi iliyopigwa Jumapili dhidi ya vinara hao wa Ligi Kuu, Simba wanaodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa.

Hata kama Simba itafanikiwa kumchukua beki huyo, kikosi chake hakitakuwa na pengo kwa sababu wapo mabeki wengine ambao wanauwezo na uzoefu wa kukabiliana na ushindani wa mechi za Ligi Kuu. Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe.

Kiungo na nahodha huyo wa zamani wa Simba alisema pia katika dirisha dogo anahitaji kuboresha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji na tayari ameshawasilisha barua kwa Wekundu wa Msimbazi akiwahitaji Juma Luizio na Jamal Mnyate.

Kwasi ana mkataba wa mwaka mmoja na Lipuli utakaomalizika mwakani na tayari ameshaanza mazungumzo ya chini kwa chini na Simba kwa ajili ya kujiunga nayo kwenye kipindi cha dirisha dogo.

Lipuli FC, Njombe Mji FC na Singida United ambayo iko katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ndio timu tatu zilizopanda daraja msimu huu.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.