Bongo Fc


Baba neymar azua zogo safari ya neymar real

Baba wa Neymar amekataa kupiga uwezekano wa mwanaye siku moja hapo baadaye kujiunga na Real Madrid.

Nyota huyo wa Brazil (25), ameondoka Barcelona na kujiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho uliovunja rekodi wa pauni198milioni.

Lakini kumekuwa na taarifa kuwa nyota huyo hana furaha kwa miamba hiyo ya Ufaransa hivyo anataka kuondoka. Baba yake Neymar ni kama ameongeza mafuta katika moto kuhusu tetesi hiyo kwa kuwaambia Fox Sports: "Mambo yamebadilika sana.

"Kwa sasa hakuna uwezekano wa kuhamia Real Madrid na jibu hili katika kujadili uwezekano wa hilo kutokea.

"Siwezi kuzungumzia kuhusu majadiliano ya miaka mitano au sita. "Neymar kwa sasa anamkataba mrefu na PSG na ndiyo kwanza amewasili hapa. Tupo hapa kwa miezi mitatu na tayari wanazungumzia kuhusu kuondoka. Aliongeza, "Ni vigumu kuzungumzia masuala hayo kwa sasa."

Nyota huyo wa zamani wa Santos alishawahi kuzungumzia mpango wake wa kustaafu soka nyumbani.

Baba yake amesisitiza kwamba bado ajenda yake ipo pale pale, na kuongeza: "Siamini kwamba Neymar ataondoka Ulaya katika miaka nane ijayo.”


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.