Bongo Fc


Azam fc yamuuza himid mao sauzi

Habari mpya ni kwamba Azam Fc jana jioni ilikuwa iingiziwe fedha za mauzo ya kiungo, Himid Mao kwenda Bidvest ya Afrika Kusini.

Azam inaelezwa kumalizana na klabu hiyo na jana kilichokuwa kinaendelea jioni ni nahodha huyo kukubaliana masilahi yake binafsi na huenda leo Alhamisi ikawa rasmi.

Lakini ishu nyingine ni kwamba Kocha wa Azam , Aristica Cioaba bado haelewi kwanini amepewa adhabu ya kukosa mechi tatu kukaa katika benchi lakini akazungumzia usajili wa straika wake mpya Bernard Arthur kuwa ni mtu anayemjua vyema.

Mromania huyo alisema alikuwa anataka kusajili mshambuliaji mwenye kasi na ujuzi wa kufunga vitu ambavyo Arthur anavyo ambapo vitaongeza kitu tofauti katika safu yake ya ushambuliaji.

Alisema Ligi ya Tanzania inahitaji kuwa na mshambuliaji aina ya Arthur ambapo endapo ataelewana vyema na Mbaraka Yusuf wataleta matokeo mazuri kwa Azam.

Azam inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu inayoongozwa na Simba. Timu hiyo ilikamilisha mechi yake ya 11 kwa sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.