Bongo Fc


Lacazette kuikosa man united j'mosi hii

Mshambuliaji wa timu ya Arsenal, Alexandre Lacazette atakosa mchezo mkali wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchesgter United Jumamosi hii.

Kocha wa timu hiyo Arsene Wenger alisema Lacazette atakuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha ya nyonga.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alipata maumivu ya nyonga katika mchezo wa juzi usiku dhidi ya Huddersfield ambao Arsenal ilishinda mabao 5-0 kwenye Uwanja wa Emirates.

Mshambuliaji huyo alifunga bao la kwanza kwa timu yake kabla ya kupumzishwa kutokana na maumivu.

Lacazette ameumia na hatacheza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mashetani Wekundu.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.