Bongo Fc


Man utd ina pancha! itaiweza arsenal?

Wakati presha ya kupambana na Arsenal ikiwa juu, Manchester United hakujatulia kwani kuna majeruhi kadhaa.

Nemanja Matic bado hajapona maumivu ambayo aliyapata katika mchezo dhidi ya Watford na hatakuwepo katika kikosi chake wakati timu hiyo ikipambana na Arsenal.

Nyota huyo raia wa Serbia, ambaye amecheza mechi 19 kati ya 22 za Man United msimu huu alitoka nje ya uwanja wakati timu yake ilipopata ushindi wa 4-2 huko Vicarage Road Jumanne wiki hii. Nyota huyo alipata maumivu ya misuli.

Ukiachana na mchezaji huyo, kocha Jose Mourinho pia atamkosa Marouane Fellaini, ambaye ana matatizo ya goti huku Michael Carrick naye akiwa bado hajapona sawasawa.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.