Bongo Fc


Scholes awapasha nyota man united kuelekea mchezo wa kesho

Paul Scholes kaibuka na kuwaambia nyota wa Manchester United wasije wakabweteka wakati watakapokuana na Arsenal kesho Jumamosi na kusisitiza kwamba kikosi hicho cha kocha Arsene Wenger kina muziki mnene.

Arsenal imeshinda mechi 12 za karibuni katika Uwanja wa Emirates tangu Aprili na ukweli ni kwamba katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu England wameruhusu bao moja pekee wakiwa nyumbani.

Man United kwa upande wao wamekuwa wakihangaika kupata matokeo mazuri wakiwa ugenini hasa wanapopambana na timu zinazoshika nafasi sita za juu tangu kutua kwa kocha Jose Mourinho.

Man United wamepata bao moja tu katika mechi saba za timu za juu ugenini kwa Arsenal, Liverpool, Chelsea, Manchester City and Spurs tangu kocha Mreno alipochukua kikosi.

Bao walilopata lilikuwa katika mechi dhidi ya Tottenham na walilala 2-1 ugenini msimu uliopita. Na wasiwasi wa Scholes ni iwapo klabu yake ya zamani itaonyesha kiwango cha hali ya juu.

"Mechi dhidi ya Arsenal ya Jumamosi ni kubwa na wanatakiwa kujitahidi kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa,” alisema Scholes.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.