Bongo Fc


Cuper: real madrid wanamtaka mohamed salah

Na: Omary Ramsey

Meneja wa Misri Hector Cuper amedai kuwa Real Madrid wanataka kumsajili Mohamed Salah. Salah alijiunga na Liverpool akitokea AS Roma majira ya joto.

Salah mwenye umri wa miaka 25 amefunga magoli 16 katika mechi 20 akiwa na miamba hao wa Merseyside katika kampeni za 2017-18.Kwa mujibu wa meneja wa timu ya taifa wa Salah, Real Madrid wamekuwa wakimfuatlia kwa karibu sana mshambuliaji huyo kuelekea dirisha la uhamisho msimu ujao wa majira ya joto.

"Nimepokea habari zilizthibitishwa zikibainisha kuwa Real Madrid wanavutiwa na Salah, lakini tusikurupukie mambo," Cuper alikiambia ON Sport TV. "Kwangu mimi yupo kwenye nafasi nzuri kwa sasa."

Salah amesaini mkataba wa miaka mitano na Liverpool alipowasili klabuni hapo majira ya joto.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.