Bongo Fc


Mtanzania wa pili amfuata samatta ubelgiji

Mtanzania Yusufu Juma anayecheza soka nchini Marekani katika klabu ya Monroe SC, yuko kwenye maandalizi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu za Standard Liège na R.S.C. Anderlecht za Ubelgiji.

Ysuph ambaye ni mzaliwa wa Kigoma, kama atafanikiwa kujiunga na moja ya timu hizo, atakuwa Mtanzania wa pili kucheza Ligi Kuu Ubelgiji ‘Jupiler pro’ baada ya nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anaichezea KRC Genk.

“Kaka yangu ambaye ananisimamia kama wakala, amefanya mazungumzo na kufanikiwa kupata zaidi ya nafasi nne za majaribio, nitaanzia London, England na kumalizia,Ubelgiji,"anasema Yusufu, kwa mujibu wa Gazeti la Mwanaspoti Jumatatu hii.

“Nacheza ngazi ya juu kabisa ya soka la Marekani upande wa vyuo baada ya hapo nitaingia kwenye mchakato wa kucheza ligi kuu. Binafsi sivutiwi na ligi kuu ya hapa Marekani, ndiyo maana naenda kufanya majaribio huko.”

Yusufu ambaye anazaidi ya miaka mitano Marekani anasimamiwa na kaka yake, Hamisi pamoja na mdogo wake ambaye yupo kwenye kituo cha kulelea vipaji nchini humo cha New England Revolution.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.