Bongo Fc


Wenger: arsenal haikuwa thabiti dhidi ya manchester united

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa timu yake "haikuwa na maamuzi thabiti" katika mechi waliyofungwa 3-1 na Manchester United.

The Gunners walikuwa wameshafungwa 2-0 katika dakika 15 za mwanzo kwa mabao kutoka kwa Antonio Valencia na Jesse Lingard, lakini Alexandre Lacazette aliwapatia bao Arsenal waliokuwa nyumbani.

Lingard alikwamisha wavuni bao la tatu akipokea pasi kwa Paul Pogba na kufanya ubao wa matokeo kusomeka 3-1, na Wenger amekiri kuwa Arsenal walikuwa na nafasi za kutosha kurudi mchezoni.

"Nadhani hatukuanza vizuri kabisa kwa upande wa ulinzi na tuna hatia kwa hilo," Mfaransa huyo aliiambia BBC Sport. Licha ya kufungwa 2-0 mapema tulipaswa kurejea mchezoni, tulikuwa na nafasi nyingi. Tulicheza katika ubora wetu, lakini hatukuwa na maamuzi thabiti.

"Kisaikolojia lilikuwa ni pigo kubwa kuruhu kichapo cha 2-0 mapema - hasa ikizingatiwa tupo nyumbani. Huenda akili zilihama mchezoni.

"Lilikuwa ni fumbo naam (kutoweza kufunga), lakini David de Gea alikuwa nyota wa mchezo kwa maili nyingi tu."

De Gea aliondosha hatari 14 katika mechi kuwazuia Arsenal kufunga, ikiwa ni pamoja na kuokoa hatari za Lacazette na Alexis Sanchez.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.