Bongo Fc


Mabao yamtajirisha kichuya





Huyo Shiza Kichuya achana naye. Mshambuliaji huyo wa Simba, kumbe si mkali wa mabao tu, hadi kwenye uwekezaji nako anapiga mabao.

Kwa Kichuya kila mkwanja anaovuta, unatumika ipasavyo katika uwekezaji.

Kichuya aliyeifungia Simba mabao 17 ya Ligi Kuu Bara tangu alipojiunga nayo msimu uliopita, mpaka sasa anamiliki viwanja viwili na nyumba, vyote vikiwa katika Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu wa Meneja wake, Profesa Midundo Mtambo, dau la usajili alilopata Simba, lilitumika kununulia viwanja hivyo huku akinunua nyumba kwa fedha zake nyingine.

Alisema kwa aina ya uchezaji wake, anaamini anaweza akabadilisha maisha kupitia kipaji cha soka, huku akimfunda asije akakengeuka nakujiona anajua kila kitu.

Lakini kuhusiana na msimamo wake juu ya wapi Kichuya atasaini na dau lake litakuwa kiasi gani, meneja hiyo alisisitiza kusubiri mkataba wa sasa umalizike kabisa ndipo watachagua timu itakayomnufaisha.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.