Bongo Fc


Ahadi 10 za mo dewji kwa klabu ya simba

Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohamed ‘Mo’ Dewji, ameelezea mipango yake kwa mwaka wake wa kwanza kuwekeza kwenye klabu hiyo baada ya kufikia makubaliano hayo ya kununua hisa asilimia 50 za klabu hiyo kwenye mkutano mkuu wa dharura uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Zabuni ya klabu hiyo, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Thomas Mihayo, kuwa mshindi wa zabuni ya kununua hisa asilimia 50, Dewji alisema katika kipindi cha mwaka mmoja, ametoa ahadi kumi kwa klabu hiyo ya Simba.

1. Kambi ya Simba itajengwa upya kabisa na itakuwa ni hosteli ya kisasa yenye vyumba hadi 35. 30 vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili ya benchi la ufundi.

2. Simba sasa itafaidika kwa kuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji.

3. Wachezaji, makocha na viongozi watakuwa na mgahawa wao wa kisasa kabisa.

4. Mo Dewji anaamini timu lazima iwe na viwanja vya mazoezi. Hivyo ataanza na viwanja viwili, kimoja nyasi asilia na kingine nyasi bandia.

5. Mo Dewji ameahidi kuwekeza katika soka la vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.

6. Mo Dewji amesema atasimamia wachezaji kuitambua thamani ya Simba kwa kujituma hasa.

7. Simba itaanza kufanya mambo kimataifa kwa kuitangaza na kuikuza brand ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika ufunguo na kadhalika.

8. Ameahidi kutenga kitita cha Sh milioni 500 ambazo zitatumiwa na benchi la ufundi katika mipango yao kama kambi na kadhalika pia Sh bilioni moja kwa ajili ya usajili.

9. Kushindana na timu kubwa Afrika na sio Tanzania pekee.

10. Kurejesha Simba katika historia ya kimataifa


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.