Bongo Fc


Ndombolo ya msuva hadi morocco

Nyota wa Difaa El Jadida ya Morocco, Saimon Msuva ambaye ni Mtanzania, ameibuka na jipya baada ya kudai kuwa zile staili za kucheza ndombolo pindi akifunga bao, sasa anazihamishia nchini humo.

Msuva alikuwa akisifika kwa kuyakata mauno pindi akitupia bao enzi zake akicheza Yanga, jambo ambalo amesema sasa litahamia nchini Morocco.

“Nilipitia THT ndiyo maana nimekuwa nikipenda sana kucheza, bado sijaanza kuonyesha vitu hivyo huku ila siku sio nyingi Wamorocco wataanza kuona, huku nipo ugenini hivyo ni muhimu kusikilizia kwanza,” alisema Msuva.

Msuva, ambaye amewahi kushinda mataji manne ya Ligi Kuu Bara, alisema ameshavizoea vyakula vya Morocco ambavyo vipo tofauti kimapishi na vyakula vingi ambavyo alikuwa amevizoea Tanzania.

“Mwanzoni ndiyo nilianza kwa kupata shida, ujue kitu ukikizoea halafu itokee ukiache na uanze kingine kidogo inahitaji muda ili kukizoea,” alisema Msuva, aliyewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu mara mbili tofauti.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.