Bongo Fc


Liverpool yajitosa kwa aubameyang

Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang ametajwa kutakiwa Liverpool huku kocha Jurgen Klopp akiwa tayari kumuachia Daniel Sturridge kuondoka.

Mshambuliaji huyo wa Gabon amekuwa na hamu kubwa ya kuondoka Borussia Dortmund msimu huu amekuwa katika wakati mgumu pamoja na kuwa amefunga mabao 17 katika mechi 19.

Aliondolewa katika kikosi cha timu hiyo kilichokwenda Barcelona kabla ya kupewa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Schalke mechi iliyomalizika kwa sare 4-4.

Gazeti la Daily Express limedai kuwa Liverpool ipo tayari kumnyakuwa nyota huyo.

Taarifa zinadai kuwa Daniel Sturridge ataondoka Anfield ili kutafuta timu itakayompa nafasi ya kucheza na kujihakikishia nafasi ya kucheza Kombe la Dunia.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.