Bongo Fc


Mourinho: matic hatacheza dhidi ya cska moscow

Bosi wa Manchester United Jose Mourinho amesisitiza kuwa kiungo wake Nemanja Matic hayupo kwenye mipango ya mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya CSKA Moscow.

Katika mechi ya wikiendi, Matic alicheza dakika zote 90 - licha ya kuingia dimbani akiwa hayupo vizuri na United waliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates.

Hata hivyo, Mourinho amemtoa Matic kwenye mechi ya Jumanne itakayopigwa Old Trafford kwa sababu ya majeraha, na amekiri kuwa Mserbia huyo pia atapata faida ya kupumzika.

Kocha huyo aliwaambia waandishi: "Tuna matatizo, tuna majeruhi. Matic amepata majeraha na ninaposema amejeruhiwa, amejeruhiwa.

"Sitamchezesha kesho kwa hiyo Matic nje. Vijana wengine wanacheza kila mechi kwa hiyo wanahitaji pia kupumzika. Muhimu zaidi, wengine nao wanastahili kupewa fursa ya kucheza."

Matic ameanza mechi 20 akiwa United katika michuano yote tangu ajiunge na klabu hiyo kutoka Chelsea majira ya joto.


Facebook Twitter

Newsletter                           

Subscribe to our newsletter for good news, sent out every time we post.